Wednesday, August 29, 2012

Kanisani kwa kina naniliu.....

Leo kanisani baada ya ibada mapasta watatu walikutana,wakaanza kuongea matatizo yao waombeane;

Pasta 1:"Tatizo langu ni wizi,kila baada ya ibada lazima niibe sadaka zinazotolewa na waumini,pliz niombeeni niache hii tabia."

Pasta 2:"Tatizo langu ni wanawake,kila mwanamke ninayemuona natamani kulala naye,nimelala na mwalimu wa sunday school na karibia waimbaji wote wa kwaya.pliz niombeeni niache hii tabia."

Pasta wa tatu akaanza kulia,wenzake wakamuuliza,"Wewe vipi?"
Akajibu:"Mi tatizo langu ni Umbea! Tukitoka hapa lazima nikaaenze kila kitu mlichosema,niombeeni jamani hii tabia niache."

Nani yuahitaji maombi zaidi?

0 comments:

Post a Comment