Thursday, August 30, 2012

SAKATA LA TID KUTAKA KUMUUA ALI KIBA.





Habari zilizosambaa kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ni juu ya sakata la msanii TID kutaka kumuua msanii mwenzake Ali Kiba kupitia kwa watu ambao walidai kuwa wametumwa na TID. Watu hao ambao walikamatwa na jeshi la polisi wanadai walikutana na mwanamuziki TID maeneo ya Mtongani ambako ndiko walikopanga mipango hiyo ya kutaka kumuua Ali kwasababu ambazo watu hao hawakuziweka wazi, Baada ya hapo ndipo walipofika maeneo anayoishi Ali kwa ajili ya
tukio hilo lakini waliweza kushitukiwa baada ya watu wa karibu wa Ali kutonywa na kufanikiwa kuwakamata watu hao baada ya polisi kufika eneo hilo.

 Watu hao walipokamatwa walimtaja TID ndiye aliyewatuma ambaye masaa machache baadaye naye alitiwa nguvuni kwa tuhuma hizo. Akiwa kwenye kituo cha polisi TID alikana kuhusika na njama hizo huku akisisitiza kuwa hana ugomvi wowote na msanii mwenzake huyo na hakuwepo nchini kwa kwani alikuwa South Africa kwa shughuli zake za kimuziki na anawashanga watu hao kumhusidha yeye na tukio kama hilo.
Hii hapa sauti yake mtu mzima T.I.D

0 comments:

Post a Comment